Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Kifo cha Imam Khomein yaliyofanyika katika Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-Salam - Tanzania kwa kuhudhuria na mamia ya watu akiwemo Mheshimiwa Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania. - Imam Khomein (ra) alikuwa kiongozi bora wa aina yake aliyepigania uislamu katika zama zote za uhai wake na akafanikiwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kuasisi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo mpaka leo hii inaendelea kufanya vizuri na kuwa Serikali ya kuigwa na mataifa mengi duniani kutokana na hatua zake za kimaendeleo na daraja za juu ambazo taifa hili limeweza kuzifikia katika nyanja mbalimbali za Kijeshi, Kisiasa, Kiuchumi na kijamii. Imam Khomein (ra) anakumbukwa kila kona ya dunia kutokana na kujulikana kwake kuwa mtetezi wa wanyonge popote walipo Ulimwengu hususan kadhia ya Waislamu wa Palestina na Wapalestina kwa ujumla.
Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Kifo cha Imam Khomein -Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-Salam - Tanzania
Hapa chini tumekuwekea picha zaidi za tukio hili
Your Comment